GET /api/v0.1/hansard/entries/1194871/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194871,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194871/?format=api",
    "text_counter": 186,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sotik, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Francis Sigei",
    "speaker": null,
    "content": "Kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika nchi hii ni jambo la maana sana. Ningependa kuchukua hii nafasi kushukuru muanzilishi wa Taifa la Tanzania, Marehemu Nyerere, kwa kufanya jambo la maana sana. Alivyoanzisha utumizi wa lugha ya Kiswahili kwa nchi hiyo, alihakikisha wananchi wanaongea hiyo lugha. Tunajua kwamba umoja wa Tanzania ni dhabiti. Kuna Wakenya ambao wamechangia katika ubunifu wa lugha ya Kiswahili, mmoja wao akiwa marehemu Ali Mazrui aliyeandika vitabu. Pongezi kwake. Tungependa kuwa na watu kama hao. Jambo la maana kwa Baraza la Kiswahili ni kutoa mwelekezo, mikakati na namna ya kutumia lugha hii. Tungependa kulipatia nafasi hili kupanga hayo mambo. Tukipata baraza la Kiswahili, tutaweza kupata mwelekeo wa lugha ya Kiswahili. Naomba tushukuru wananchi wa Kenya. Wengi wanasubiri hii lugha iwe lugha ya taifa. Shida tuliyonayo ni mwelekeo na namna ya kutumia lugha sanifu. Lugha tunayoijua ni sheng . Mhe. Yussuf, tungependa uchukue hatua nyingine ili ulete Mswada. Lugha inayotumika mahakamani ni Kiingereza. Najua kwamba wanaohukumiwa wanahukumiwa bila kujua lugha iliyotumika. Wanaambiwa waaende jelani au wamepigwa faini halafu wakili wake anamueleza yaliyojiri. Inafaa tuanze kuchukua nafasi hii kama Serikali tuone kwamba lugha ya Kiswahili inatumika. Hata Kanuni za Kudumu tunafaa kuzitumia zile za lugha ya Kiswahili."
}