GET /api/v0.1/hansard/entries/1194877/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194877,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194877/?format=api",
    "text_counter": 192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kenya kama lugha ya Taifa. Kiswahili kama lugha ya Taifa katika nchi yetu ya Kenya haijatiliwa maanani. Hakijaheshimiwa kulingana na vile kimetambuliwa kama lugha ya Taifa. Kukibuniwa Baraza hili, basi, litaweka mikakati dhabiti ambayo itasababisha lugha hii yetu ya Kenya iweze kupendwa; iweze kuwa na watu wengi ambao wanaienzi na watu wanaojivunia lugha ya Kiswahili. Kiswahili ni lugha ambayo inaweza pia kutumika kuunganisha Wakenya. Tunajua vyema ya kwamba yako makabila mbalimbali lakini kuna jambo moja ambalo linaweza kutuunganisha. Lugha ni mojawapo ya mambo ambayo yanaweza kuunganisha watu. Lugha ya Kiswahili inaweza kutuunganisha. Na sio Kenya pekee yake bali Africa nzima. Hata Africa Mashariki tunaweza kuunganishwa na lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hii nikisema ni wakati wa usawa. Ya kwamba huu mpango mzima wa kubuni hili Baraza uweze kufanyika ili lugha hii iweze kutukuzwa katika Kenya nzima. Namshauri pia Mhe. Yusuf Hassan kwa kumueleza, baada ya hapa, tumekuwa tukizungumza hapa Bungeni na mara nyingi yanaishia hapa. Basi ni wakati tuweze kuenda hatua nyingine tena baada ya hapa tufuatilia yale tunayoyanena hapa tuyatende. Tuhakikishe kwamba lugha ya Kiswahili inazungumzwa na watu wanajivunia. Kuwe na mikakati bora na watu waweze kujifunza ili tuweze kuimarisha Kiswahili na kiwe bora katika nchi yetu na tuweze kuwa na Kiswahili cha kutuunganisha kama Wakenya."
}