GET /api/v0.1/hansard/entries/1194882/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194882,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194882/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ganze, PAA",
    "speaker_title": "Mhe. Kenneth Tungule",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nitoe maoni yangu kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili hapa nchini Kenya. Pia nachukua fursa hii kumpongeza Mbunge wa Kamukunji, Mhe. Yusuf Hassan, kwa kuleta Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili hapa nchini Kenya. Kama vile wenzangu wametangulia kusema, ni kweli kabisa kuwa Kiswahili ni lugha ambayo inadhaminiwa sana hapa Kenya na watu wengi. Ni lugha ambayo inatumiwa na makabila karibu yote hapa Kenya. Sio Kenya pekee yake, lakini ukiangulia ukanda wote wa Africa Mashariki, ukanda wote wa Maziwa Makuu na Afrika nzima kwa jumla, sasa wamekubali lugha ya Kiswahili na wameanza masomo mbalimbali katika nchi zao kuhakikisha kuwa lugha inabobea katika nchi hizo. Lakini la kushangaza hapa nchini Kenya bado tunachukulia lugha ya Kiswahili kama lugha dhaifu kwa sababu wengi wanafikiria mtu akiongea Kiswahili huwa hajasoma vizuri ama ana elimu duni. Wananchi wa Kenya huwa wanashabikia Kiingereza sana kuliko hii lugha yao ambayo imetambuliwa na Katiba ya Kenya kama lugha ya Kitaifa. Pale Pwani ninakotoka, lugha ya Kiswahili inakejeliwa sana, hata ukiangalia kwenye mitihani ya Kitaifa ya Darasa la Nane na Kidato cha Nne. Ukiangalia vile wanafunzi wanavyofanya mitihani yao ya lugha ya Kiswahili, utapata hawapati alama nyingi sana ijapokuwa inasemekana wazi kwamba Pwani wanaongea Kiswahili. Lakini hali hii haionekani katika ile mitihani ya Kitaifa. Utapata wanaopita vizuri mtihani ya Kiswahili huwa ni shule za kutoka sehemu ya Bara wala siyo sehemu ya Pwani. Hili ni jambo ambalo ni lazima kama viongozi tulitilie maanani na ndio maana nasimama hapa kuunga mkono Hoja ya Mhe. Yusuf Hassan ya kusema ni lazima tubuni"
}