GET /api/v0.1/hansard/entries/1194884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194884,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194884/?format=api",
    "text_counter": 199,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Baraza la Kitaifa ili tuweze kuhamasisha Wakenya tukijumuisha hata Wapwani ili waweze kuongea hii lugha na waweze kuisanifisha na kuongea kama vile ndugu zetu kule Tanzania tunawaona wakiongea. Hii lugha tukitumia vizuri inaweza kuunganisha Kenya. Tuna makabila zaidi ya 45 na kila kabila lina lugha yake. Tanzania wana makabila zaidi ya 50 lakini sio rahisi kujua Mtanzania ni wa kabila gani kwa sababu wote wameunganishwa na lugha ya Kiswahili. Naomba kama inawezekana, Baraza la Kitaifa hapa nchini liundwe ili liweze kuleta Wakenya wote pamoja ili waweze kusahau makabila yao, waweze kuwa na lugha moja ambayo itawaunganisha wote kama Wakenya. Mhe. Spika wa Muda, lugha ya Kiswahili haiongewi hapa Kenya pekee yake. Kama nilivyosema, hata Bara ya Ulaya na Uchina wanatumia Kiswahili. China wameandika walimu wengi wa Kiswahili wanaowafunza wananchi wao jinsi ya kuongea Kiswahili. Ukienda kule Marekani pia, utaona walimu wengi wa Kiswahili wamepelekwa huko. Wanafunza Wamarekani jinsi ya kuongea Kiswahili. Utaona kuna wasanii waliobobea Wamarekani ambao wameimba nyimbo kwa lugha ya Kiswahili. Msanii kama Michael Jackson aliwahi kuimba nyimbo kwa lugha ya Kiswahili. Msanii kama Lionel Richie pia aliimba wimbo katika lugha ya Kiswahili na hao ni Wamarekani. Msanii Rihana ameimba nyimbo katika lugha ya Kiswahili. Lakini hapa Kenya, sisi wenyewe tunadhalilisha lugha ya Kiswahili. Watu wanatoka nchi za mbali kuja Kenya kusoma lugha ya Kiswahili. Kuna wanafilamu waliobobea kutoka Marekani pia kama vile akina Forest Whitaker walikuja hapa Afrika, Uganda, wakasoma Kiswahili na wakatengeneza filamu kama vile The Last King of Scotland . Ni Wamarekani lakini wanaongea lugha ya Kiswahili na wanaongea Kiswahili sanifu. Kwa hivyo, mimi naunga mkono Hoja hii ya Mhe. Yusuf Hassan ya kuwa hapa Kenya pia tubuni Baraza la Kiswahili ili tuweze kuhakikisha Wakenya wanaongea lugha sanifu. Hapa Nairobi najua kuna shida kubwa sana kwa sababu wanaingiza sheng kwa Kiswahili kila wakati. Wenyewe wanasema ni Kiswahili lakini mtu ambaye anatoka Pwani akisikia vile wanaongea pengine hataelewa hata neno moja ambalo linaongewa pale. Kiswahili kinaunganisha wananchi na kinaleta identity na uniformity. Hii itawezekena kama kutakuwa na baraza rasmi ambalo litakuwa linahakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inapewa kipaumbele. Inahitajika ili iweze kuwa lugha nzuri. Na sio lugha rasmi pekee yake, lakini pia iwe lugha nzuri ambayo inakubalika kila pembe zote za Kenya. Kwa hayo machache, ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Nazidi kupongeza hatua ya Mhe. Yusuf Hassan kwa kuhakikisha kuwa Baraza la Kitaifa ya Kiswahili litabuniwa hapa nchini Kenya. Ahsanteni sana."
}