GET /api/v0.1/hansard/entries/1194886/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194886,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194886/?format=api",
    "text_counter": 201,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Saboti, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Caleb Amisi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi mwafaka ya kujadili Hoja hii. Nampongeza rafiki yangu, Mhe. Yusuf Hassan, kwa kuwa na hekima ya kuleta Hoja kama hii. Lugha ya Kiswahili na lugha ya Kimombo zimeorodheshwa kama lugha rasmi za kitaifa katika Katiba yetu ya Kenya. Lakini miaka kumi na miwili imeisha na hatujaweza kuitafsiri Katiba hiyo ikawa katika lugha ya Kiswahili vile ilivyo katika lugha Kimombo. Hicho ni kinaya - kwamba tumeiweka lugha ya Kiswahili kipao mbele katika Katiba ilhali hatujapata nafasi ya kutafsiri Katiba ya Kenya katika lugha ya Kiswahili. Nikikumbuka wale ambao wako na umri kama huu wangu ambao wametoka shule hivi majuzi, kuna vile vitabu tumesoma. Kuna wale ambao walibobea katika lugha ya Kiswahili na wakawa mstari wa mbele kukuza Kiswahili. Mfano ni yule aliyekuwa anatambulika, marehemu Ken Walibora. Wale wanakumbuka Ken Walibora - Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - alikua mstari wa mbele kuikuza lugha ya Kiswahili. Tulimpoteza na hakuna mahali tunamkumbuka. Ni vizuri tungekuwa tunawakumbuka watu kama hao ambao wamekuwa"
}