GET /api/v0.1/hansard/entries/1194888/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194888,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194888/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "mstari wa mbele. Wale wanaokumbuka kitabu cha Siku Njema, siku njema itakuja lini? Ni kitabu ambacho kilisifika sana kwa wale walikuwa kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule za upili. Ni kitabu ambacho kilibuniwa na kupaliliwa katika masomo na hata mtihani wa kidato cha nne. Unakumbuka pia tulikuwa na Wala bin Wala na yule aliandika kitabo cha wale ni sisi na sisi ni wale. Yaani Walenisi . Wanaokikumbuka hicho kitabu, kilikuwa na hekaya na riwaya ambayo ukiisoma unapata kusisimka na inasisimua akili yako. Kimeandikwa kwa njia ya kukejeli lakini kina mafunzo. Wale wanakumbuka hivi vitabu, vilitufunza mambo mengi tukiwa katika shule za upili na tulitahiniwa. Unakumbuka kulikuwa na wanafunzi wanapenda kusoma hivi vitabu na kufurahia. Lakini tukishamaliza mtihani, huo ndio ulikuwa mwisho wa Kiswahili. Hatuendelei kukuza lugha ya Kiswahili ili tuweze kuiweka mbele kama lugha ya kitaifa. Pia kuna kitabu ambacho kilijulikana kama Kitumbua Kimeingia Mchanga. Ni kitabu ambacho kilisifika sana. Hatujawahi kuwasifu wale wameandika vitabu hivi. Hatujawaweka mstari wa mbele. Tunaongea kuhusu kubuni Baraza la Kiswahili la Kenya. Tungewaweka hao katika Baraza hilo ama kitengo cha kushughulikia maswala ya Kiswahili, na hivi tungeiweka Kiswahili mahali panapofaa."
}