GET /api/v0.1/hansard/entries/1194889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194889,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194889/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, leo asubuhi nimekuwa na mkutano na raia wa Uingereza. Ingekuwa jambo kubwa kwamba huwezi kupata Mkenya akisema anasomea somo la Kiswahili. Lakini inanishangaza kwamba huyu Muingereza amekuja hapa hivi maajuzi, hajamalizia hata mwezi mmoja, lakini anakwambia: “Niko katika somo la Kiswahili. Najifunza lugha ya Kiswahili”. Itakuwaje kwamba wale wa nchi za ughaibuni wanatamani sana lugha yetu? Wanapofika hapa, jambo la kwanza wanalokuambia ni ‘naam’ na ‘ahsante’, kwa kuwa wameshajifunza. Wanajua kwamba ukifika Kenya, hata balozi anapotumwa Kenya, salamu za huko ni ‘ahsante’. Wameshajua kwamba Kenya na Kiswahili ni moja. Lakini sisi hapa hatuitambui lugha hii ila nchi nyingine zinaitambua lugha ya Kiswahili. Wao wana hamu sana ya kuisoma na kuingia shuleni wakitaka kufahamu hii lugha kwa undani. Hiki ni kinaya kikubwa sana. Pia, twafaa kuweka vyuo vikuu viwe na vitengo mwafaka vya Kiswahili ili wanafunzi wanapojifunza lugha ya Kiswahili, wajue mwishowe watapata kazi. Watasema tulikua tunaimba: ‘Someni vijana, mwisho wa kusoma mtapata kazi nzuri sana.’ Lakini sasa watu hawajui ikiwa watapata kazi baada ya kusoma. Watu wanajua baada ya kusoma ni giza na hakuna kazi. Sasa inafaa tujue kwamba tukiviweka vyuo vikuu vya kusomesha Kiswahili, wanafunzi watajua wakisoma somo hili la Kiswahili wataingia chuo kikuu na watakua walimu wa lugha ya Kiswahili. Chambilecho wahenga: Cha mkufuu mwanafuu ha, na akila hu; cha mwanafuu mkufuu hu, na akila ha. Ahsante sana."
}