GET /api/v0.1/hansard/entries/1194892/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194892,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194892/?format=api",
    "text_counter": 207,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Turbo, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Janet Sitienei",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nichangie Hoja hii. Kwanza kabisa napenda kumpa kongole Mheshimiwa wa Kamukunji kwa kuleta Hoja hii. Hakika, katika karne ya ishirini na moja, ni bora kutukuza lugha ya Kiswahili ili itumike sehemu zote nchini. Pia, sisi kama Wabunge twafaa tuwe na uzoefu wa kutumia lugha hii ya Kiswahili katika mijadala yetu. Hii ni ili wenye-nchi wetu - wakiwemo wazee, akina mama, vijana, pamoja na watoto - waweze kuelewa ni nini kinachoendelea bungeni. Nikitambua Kifungu cha Saba cha Katiba ya Kenya kinabainishia Serikali kulinda, kuendeleza ama kukuza matumizi ya Kiswahili, ningependa kuunga mkono Hoja hii ili iboreshwe kwa manufaa ya sisi wananchi wa Kenya."
}