GET /api/v0.1/hansard/entries/1194894/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194894,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194894/?format=api",
"text_counter": 209,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ilani",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mkutano wa mwaka wa 2021 wa Marais wa Umoja wa Afrika Mashariki walikubaliana kubuni tume ya baraza la Kiswahili. Basi hatuna budi kuunga mkono kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya kwa sababu hii itarahisisha wananchi kupata mawasiliano kamili. Pia itaboresha kufuzu kwa wanafunzi wetu wa kidato cha nne na kuingia chuo kikuu. Katika baadhi ya mahitaji ama masomo yanayohitajika kuingia chuo kikuu, wanaangalia sana lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa muda, kubuniwa kwa baraza hili kutasaidia zaidi. Nakumbuka wakati mmoja nilipigia mkaaji wa Mombasa simu. Nilipopiga simu, aliniuliza: “Ni nani mwenzangu?” Sikuelewa anamaanisha nini. Nilishinda nikimuambia: “Hapana! Mimi ni Janet!” Naye ananiuliza: “Ni nani mwenzangu?” Sikuelewa alimaanisha “ni nani anaongea”. Kwa hivyo, ni muhimu sana kuweza kukuza lugha ya Kiswahili ili isaidie watu wengi. Itaboresha hata wanabiashara katika nchi ya Kenya. Kuna asilimia kubwa ya wanabiashara ambao hawawezi kuelewa ama kuzungumza lugha ya Kiingereza. Kwa hivyo kubuniwa kwa baraza hili itawawezesha kuweka mikakati bora ambayo itawasaidia wananchi wengi na kuwasaidia wafanyabiashara katika mawasiliano yao. Hivyo, uchumi wetu utakuzwa kupitia mawasiliano bora. Kubuniwa kwa baraza hilo kutachangia uhusiano, kuungana pamoja na mawasiliano bora kwa wenyeji wa Afrika Mashariki. Nasimama hapa kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa hapa Bungeni na mwenzangu Mhe. Yusuf, Mbunge wa Kamukunji."
}