GET /api/v0.1/hansard/entries/1194898/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194898,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194898/?format=api",
    "text_counter": 213,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Tigania East, NOPEU",
    "speaker_title": "Mpuru Aburi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Kiswahili ni lugha ya maana sana kwa Wakenya wenzangu. Kwa sababu, ukiangalia kule mashinani, wakati tunakimbia huku na kule kuomba kura, hatutumii Kiingereza. Tunatumia Kiswahili. Siku hizi, hapa nchini Kenya, kila mtu ana runinga ndani ya nyumba yake. Lakini kule mashinani wanaoelewa Kiingereza ni wachache. Hata wenye pikipiki wakiwa na simu zao mkokoni husikiliza stesheni ya Bunge. Wabunge walikimbia huku na kule kuomba kura lakini hapa Bungeni, tunazungumza Kiingereza tu. Tukienda kunywa chai pale nje, hakuna yeyote anayeongea Kiingereza. Ni Kiswahili peke yake. Ndiyo maana naunga mkono ndugu yangu Bw. Hassan, kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Hii ni kwa sababu hakuna njia nyingine ya kuunganisha Wakenya ama mtu aliyesoma na yule hakusoma ila ni kupitia Kiswahili tu."
}