GET /api/v0.1/hansard/entries/1194899/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194899,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194899/?format=api",
"text_counter": 214,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tigania East, NOPEU",
"speaker_title": "Mpuru Aburi",
"speaker": null,
"content": "Tukiangalia mambo ya mashamba, maofisa kutoka Wizara ya Lands yani makarani, huenda mashinani kushugulikia mambo ya mashamba. Wakifika huko, wanaongea Kiingereza tu hata katika kesi zote za mashamba. Mzee na mama hawaelewi; wanatingisha vichwa tu. Kumbe hapo wanakuliwa na hao makarani. Ndiyo nasema Kiswahili ni lugha ya maana sana. Ukiangalia wenzetu Watanzania, wanazungumza Kiswahili na kimewaunganisha wote. Mtanzania hajali kabila lake ni gani. Yeye anajua ni Mswahili na hawezi kuzungumza lugha nyingine ila Kiswahili tu."
}