GET /api/v0.1/hansard/entries/1194900/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194900,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194900/?format=api",
"text_counter": 215,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tigania East, NOPEU",
"speaker_title": "Mpuru Aburi",
"speaker": null,
"content": "Lakini hapa nchini Kenya, ukienda kwenye ofisi za Serikali, unawapata watu wanazungumza Kiingereza. Hakuna lugha nyingine. Hata mtu akiwa anataka kuwaeleza kitu cha maana anashindwa, au kuskia aibu kwa sababu hatasikilizwa. Ukienda kortini au kwenye magereza kwa mfano Kamiti ama rumande huko Industrial Area, asilimia 80 ya wafungwa ni watu hawana makosa yoyote. Wakifika kortini, jaji, wakili na prosecutor wanazungumza Kiingereza. Sasa huyo jamaa anapanua mdomo tu mpaka anapelekwa ndani."
}