GET /api/v0.1/hansard/entries/1194919/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194919,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194919/?format=api",
    "text_counter": 234,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dagoretti Kusini,UDA",
    "speaker_title": "Mhe. John Kiarie",
    "speaker": null,
    "content": " Nakushukuru sana, Mhe. Spika wa Muda. Siichukulii nafasi ya kuchangia Hoja hii kwa wepesi. Ningependa kwanza kumpongeza sana ndugu yangu ambaye pia ni Mjumbe wa Eneo Bunge lililo hapa mjini katika Kaunti ya Nairobi. Nampongeza sana Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya maana zaidi. Nafahamu kuwa Mhe. Yusuf Hassan ni mwanahabari anaye uzoefu mkubwa katika uhariri wa habari. Ni desturi na historia yake iliyomshawishi kuleta Hoja hii muhimu ya kutupendekeza tubuni Baraza la Kiswahili hapa nchini. Kwanza kabisa, nampongeza Mhe. Yusuf Hassan kwa wazo hilo bunifu na la maana zaidi kwa nchi yetu na lugha tukufu ya Kiswahili."
}