HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194921,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194921/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ilani",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mwimbaji wa wimbo aliimba na kusema Kiswahili kitukuzwe kwani ni lugha ya Taifa. Akasema pia watu wanapokutana bila lugha, watakwama. Hakika, chambilecho wahenga, mwacha mila ni mtumwa. Kunaye msomi tajika kwa jina la Leo Mohammed ambaye hufunza desturi za jamii, watu na mataifa. Katika mafunzo yake, mwalimu Leo Mohammed anatushawishi kwamba adui wa mtu ni mtu. Anatushawishi pia kuwa anayetaka kukutelekeza, kukupokonya na hata kukutia utumwani, jambo analofanya kwanza ni kukunyang’anya lugha yako. Mwalimu Leo Mohammed hufunza kwamba yeyote anayetaka kukufanya mtumwa, huwa kwanza anakunyang’anya jina la babako. Jina la babako ndilo hubeba asili yako. Kisha, anakunyang’anya lugha ya mamako kwa sababu hapo ndipo culture yako ipo. Hapo ndipo utamaduni wako upo. Anasema kwamba ni vizuri yeyote anayependa kuzingatia utamadani wake ahifadhi lugha yake. Nina hofu sana kwa sababu nchi yetu inatajika duniani nzima kwa sababu ya wanariadha wetu wanaotuletea sifa kuu. Lakini wanaposhinda na kukutana na wanahabari, huwa tunawaona wakijikanganya na lugha za kigeni. Wanapofanya hivyo, yule ambaye alikuwa amepata hadhi ya juu sana kwa kushinda mbio za riadha, anashushwa hadhi kwa sababu anajaribu kuongea kwa lugha ya kigeni. Anapojaribu kuongea lugha ya kigeni, anakanganywa na ile ambayo tunaita lafudhi – athari za lugha ya mama. Hii ni kwa sababu wengi wao wanatoka katika sehemu za Bonde la Ufa na Mlima Kenya. Wakijaribu kuongea lugha za kigeni, lafudhi inawatatiza, na wanapata athari kubwa sana za lugha ya mama. Napendekeza kuwa kupitia Baraza hili litakalobuniwa, tuwahimize wanariadha wetu kwamba lugha yao iwe ni Kiswahili. Yule ambaye anataka kumhoji ajifunze lugha yetu. Wagiriki wakishinda, wanaongea lugha yao. Wafaransa wakishinda, wanaongea Kifaransa. Huyo mwanahabari achukue jukumu la kutafsiri lugha yetu ili wanariadha wetu waweze kuhifadhi hadhi yao wakishinda mbio hizo. Wasishushe hadhi yao wakijaribu kuongea lugha zinazowatatiza. Ni jambo la kustaajabisha kwamba hapa nchini, tunaenzi mashirika na taasisi za kigeni ambazo zimebuni mabaraza ya lugha zao zilizo hapa nchini. Sio jambo baya kuwa na mabaraza hayo. Hapa Nairobi, tunazo British Council, Goethe Institute na Confucius Institute. British Council inaenzi lugha ya Kiingereza. Inaiimarisha na kuiweka katika safu za juu sana, na pia kutuhimiza tuongee lugha yao. Kwa hivyo, hili ni jambo la busara ambalo limeletwa hapa na Mhe. Yusuf. Tukiwa na taasisi yetu ambayo kazi yake ni kuhimiza watu waenzi lugha yetu, tutakuwa tumechukua hatua ya maana sana kama nchi. Pia, tutapeleka taasisi hiyo katika nchi za mbali ili tuhimize wananchi wakienzi Kiswahili. Tutakapobuni Baraza hili, itabidi tuwakumbuke wale magwiji wa lugha ya Kiswahili ambao walitutangulia. Kunao wasomi tajika. Tutaweza kumkumbuka msomi Ali Mazrui, aliyefanya kazi kubwa sana ya kuimarisha lugha ya Kiswahili na kueneza dini ya Kiislamu katika bara letu la Afrika. Tunahitaji mahali ambapo tunaweza kumuenzi msomi huyu. Kuna wasomi wa hivi punde kama vile Ken Walibora, ambaye vitabu vyake vilikuwa katika mtaala wa masomo ya nchi hii. Hatungependa kumsahau. Kando na wasomi, tuna watangazaji tajika kama Leonard Mambo Mbotela, ambaye ni gwiji wa lugha. Tunaye mwanahabari Swaleh Mdoe, na wengine wengi, ambao wameibuka kama watu tajika ambao wamemezea lugha yetu ya taifa. Baraza hilo la lugha ya Kiswahili lichukue jukumu hilo la kuwaenzi hao wasomi na magwiji wa lugha ya Kiswahili. Jambo lililonifadhaisha sana ni kuwa katika Kongamano la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wetu wa awali alikuwa Mwenyekiti katika kikao kilichopitisha hoja kuwa Kifaransa kijumuishwe katika lugha za nchi za Afrika Mashariki. Jambo hilo lilinifadhaisha sana kwa sababu katika nchi zetu za Jumuiya ya Afrika Mashariki, tuna lugha yetu ya kiasili ya Kiswahili. Hao tunaowaenzi zaidi na kutumia lugha zao, tusiwahi sahau hata siku moja kwamba walikuwa wakoloni waliotuweka utumwani. Kwa kuenzi lugha zao, tunaendeleza zile itikadi zao za kikoloni. Nahimiza Bunge hili lisimame kidete na kuiambia"
}