GET /api/v0.1/hansard/entries/1194923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194923,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194923/?format=api",
    "text_counter": 238,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Jumuiya ya Afrika Mashariki ikosoe pendekezo hilo lililopitishwa kwamba nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zitumie lugha ya Kifaransa kama mojawapo ya lugha rasmi. Tuinue Kiswahili mahali ambapo tulitaka kuweka lugha hizo za kigeni. Mwisho kabisa, kila mtu ana jukumu. Hata tunaposubiri Baraza hilo libuniwe ili tukuze lugha yetu, itatubidi sisi wenyewe tuchukue jukumu. Bunge hili litenge siku moja ya kujadiliana katika lugha ya Kiswahili. Tunazo Kanuni za Kudumu katika lugha ya Kiswahili. Kwangu nyumbani, nimewahimiza watoto wangu wajue lugha ya kiasili ya mama na wanaiongea. Pia wanaiongea lugha ya Kiswahili. Wakienda shuleni, watafunzwa Kifaransa na Kizungu. Lakini nyumbani, mimi ni mwalimu wa kwanza wa lugha na nahimiza lugha zetu zienziwe daima na daima. Ahsante sana kwa kunipa nafasi hii, Mhe. Spika wa Muda. Nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwa lugha ya kitaifa tunayoienzi sana. Kiswahili kitukuzwe."
}