GET /api/v0.1/hansard/entries/1194927/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194927,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194927/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nandi CWR, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Cynthia Muge",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii kumshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya umuhimu kabisa katika Bunge hili inayohusu kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili nchini Kenya. Kiswahili kama vile Wabunge wenzangu wamesema ni lugha ya maana sana ambayo inazungumzwa na watu wengi duniani. Naunga mkono Hoja hii nikisema kwamba tuhakikishe ya kuwa lugha ya Kiswahili imetukuzwa. Pia, pale kwenye Bunge za Kaunti, bado wanatumia Kanuni za Kudumu. Hawana chapisho kwa lugha ya Kiswahili. Hoja hii ni muhimu na itatusaidia sana. Lugha ya Kiswahili ni lugha ya kiasili ya Kiafrika na inatusaidia sisi kama Waafrika. Lugha ya Kiswahili ina heshima na hili Baraza litatusaidia tuhakikishe kwamba kila wakati tunadhibiti na kukuza lugha ya Kiswahili nchini Kenya. Nashukuru Mhe. Yusuf kwa kunipatia hii nafasi niweze kuichangia na naiunga mkono Hoja hii kwa dhati. Ahsante."
}