GET /api/v0.1/hansard/entries/1194929/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194929,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194929/?format=api",
    "text_counter": 244,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Nachukua fursa hii kumshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kunipa hii fursa ili niweze kupenyeza sauti yangu katika Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili. Naunga mkono kwa sababu wakati Baraza hili litakapobuniwa, nina imani kwamba Kiswahili kitashamiri na kitakuwa lugha muhimu katika Taifa letu. Mataifa mengi yaliyondelea yalitumia lugha za mama. Ukiangalia Uingereza, Urusi na Bara la Arabu, wanatumia lugha zao na nchi hizo zimeendelea zaidi. Ukiangalia Taifa Jirani letu la Tanzania, limeweza kuwa na maendeleo mengi kwa sababu ya kutumia lugha zao. Ningeomba kwamba almashauri zote za kiserikali ziweze kuweka maandishi katika milango kwamba unapoingia katika jumba hili, unaweza kutumia lugha mbili ambazo ni Kiingereza na Kiswahili. Lugha ya Kiswahili si mawasiliano tu mbali lugha nzuri kwa Wakenya na Afrika Mashariki na haswa Pwani ambako ni kitovu cha Kiswahili. Lugha hii ni fursa ya vitu vingi."
}