GET /api/v0.1/hansard/entries/1194934/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194934,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194934/?format=api",
    "text_counter": 249,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kamukunji, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Yusuf Hassan",
    "speaker": {
        "id": 398,
        "legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
        "slug": "yusuf-hassan-abdi"
    },
    "content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Leo tumekuwa na kikao cha kihistoria na naona kwamba tumefanikiwa katika kulizungumzia na tumekuwa na mjadala wa kusisimua. Tumekuwa na ari, mori na hamu kubwa sana ya kuweza kulizungumzia swala hili la Kiswahili. Tumetambua kwamba Kiswahili ni lugha muhimu ambayo ina hadhi na majukumu mbalimbali. Ni lugha ya kitaifa ambayo ni rasmi na ni lugha ya kimataifa. Ni dhahiri kwamba lugha hii ni muhimu sana na ina mawanda mapana ya kimatumizi kuliko lugha yoyote ya kiasili. Naomba tuipeleke mbele Hoja hii na ninataka kuweka swala hili mbele yako Mheshimiwa Spika wa Muda ili tuweze kuipeleka mbele katika Kikao kijayo. Nawashukuru wote ambao waliweza kuchangia na kulizungumzia. Nawapa hongera wanafunzi ambao wameweza kuhudhuria kikao cha kihistoria cha kwanza tangu niingie Bungeni. Nimekuwa katika Bunge la Kumi, Kumi na Moja na Kumi na Mbili. Ni mara ya kwanza ambapo tumetumia wakati mwingi kama huu kuzungumzia hii lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili. Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda."
}