GET /api/v0.1/hansard/entries/1195353/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1195353,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195353/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": " Asante Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii nichangie Hoja hii. Wazee wa mitaa ni viongozi ambao wanafanya kazi nyingi sana. Wanatatua kesi mbali mbali za kifamilia na wizi. Watu wengine wanafikiria kuwa wazee wa mitaa ni wanaume pekee yao; akina mama pia ni viongozi wa mitaa. Naunga mkono Hoja hii ili viongozi hawa walipwe na watambulike kwenye mikutano. Viongozi hawa wanafanya kazi ngumu sana kuliko ya chifu ama hii yetu. Wamesaidia taifa letu kwa muda mrefu. Pia wanafaa kuelimishwa kwa mambo ya uongozi na utendakazi wema. Sio lazima wazee wa mitaa wawe na cheti cha masomo; cheti chao ni hekima kutoka kwa Mungu. Lazima akina mama pia wapatiwe nafasi ya kufanya kazi hii. Bunge linafaa kuhakikisha kuwa wazee wa mitaa na viongozi wa Nyumba Kumi wanalipwa kwa kuwa wanafanya kazi nzuri mitaani. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}