GET /api/v0.1/hansard/entries/1195408/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1195408,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195408/?format=api",
"text_counter": 252,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika wa Muda, eneo Bunge langu la Kaloleni limeshuhudia visa vya mauaji ya wazee. Mzee akiuawa na polisi wafike, wanauliza mzee wa mtaa alikuwa wapi mtu yule akiuawa. Wazee wa mitaa wamekuwa wakihangaishwa sana lakini hakuna mtu ambaye amewahi kuwambia asante kwa ile kazi wanayofanya. Hoja hii imekuja wakati mzuri. Wasiwasi wangu ni kwamba katika mwaka wa 2018 tulipitisha Hoja kama hii inayosema kwamba ni lazima wazee wa mitaa wafidiwe lakini Hoja hiyo haikutekelezwa kwa kisingizio kwamba hakuna pesa. Safari hii tunaiomba Serikali iliyopo, kupitia Wizara ya Masuala ya Ndani na Utawala, watenge pesa maalum katika bajeti zao ambazo zitashughulikia marupurupu ya wazee wa mitaa. Hawa ndio wanaeleza Serikali shida zinazowakumba wananchi kule mashinani."
}