GET /api/v0.1/hansard/entries/1195409/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1195409,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195409/?format=api",
    "text_counter": 253,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": null,
    "content": "Hivi sasa kuna kiangazi ambacho kinawasumbua wananchi. Wazee wa mitaa na wazee wa nyumba kumi ndio wanaotumika kutoa majina ya wale watu ambao wanateseka na ukame lakini chakula kinapogawanywa, wao hawawezi kuwa katika orodha ya wale ambao wana shida ya njaa. Hili ni jambo la kusikitisha. Wazee wa mitaa wako na familia zao na watoto ambao wanatakiwa kwenda shuleni lakini hakuna msaada wowote kutoka kwa Serikali ambao wanapata ili watoto wao waende shuleni. Watoto wengi wa wazee wa mitaa na wazee wa nyumba kumi wanaendelea kubaki nyumbani. Pengine ile pesa walikuwa wanategemea ni ule mfuko wa maendeleo ya maeneo Bunge (NG-CDF), ambao bado haujapatikana sasa. Kwa hivyo, ni muhimu tuweze kuwatambua wazee wa mitaa. Ninawaomba Wajumbe wenzangu, kwa sababu wazee wa mitaa wametusaidia kwa njia moja ama nyingine na kuimarisha usalama katika maeneo Bunge yetu, waipitishe Hoja hii na pendekezo hili lishughulikiwe na kuwa sheria ili wazee wa mitaa waweze kufidiwa. Vilevile, hao wazee ni lazima watafutiwe sare maalum ili waweze kutambulika mitaani. Ningependa nguo hizo ziwekwe majina yao ili wananchi waweze kuwatambua kwa rahisi na watoe huduma kwa wakaazi kwenye mitaa wanakohudumu. Ninaomba tuipitishe Hoja hii kwa haraka ili Serikali iweze kutenga pesa mara moja za kuwasaidia hawa Wazee wa mitaa na mabalozi wa nyumba kumi."
}