GET /api/v0.1/hansard/entries/1195426/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1195426,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195426/?format=api",
    "text_counter": 270,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa muda. Nataka kuungana na wenzangu katika kuiunga mkono Hoja hii. Wazee wa mitaa ni wazee ambao wanafanya kazi kubwa sana katika maeneo ya mitaa yetu. Tukiangalia, ni wazee ambao walifanya kazi miaka yote wakisaidia katika kudumisha amani. Vilevile, kukitokea matatizo hao ndio watu wa kwanza ambao wanafuatwa. Tukiangalia kabla ya chifu, sub-chief, Assistant County Commissioner (ACC) ama Deputy County Commissiner (DCC) kujua yanayoendelea kule nyanjani, ni muhimu sana anaangalia kuuliza mzee wa mtaa. Leo katika sehemu nyingi sana, wazee wa mitaa wanafanya kazi kubwa, haswa kufuatilia masuala ya usalama. Kwa mfano, katika sehemu yangu moja ya Kitui, ambako mheshimiwa Bwire, mbunge wa Taveta, ana makao yake, utaona mzee wa mtaa anayeitwa Mzee Gona ndiye anayemwangalilia mambo yake pale. Kwa hivyo, leo hii, kama Mbunge wa Jomvu, ningependa kusema kuwa naunga mkono hawa wazee wa mitaa watambuliwe. Kama vile wanavyotambulika chief, subchief, ACC na DCC, ni muhimu pia hiyo structure iwatambue wazee wa mtaa katika sehemu zetu. Vile wanavyolipwa wengine ni muhimu pia wazee hawa watambuliwe. Hawa wazee wako na familia, wanasomesha watoto na wanaishi katika hali duni. Hawana hali ya kuweza kujikimu kimaisha na kulipa kodi ya nyumba. Ikipitishwa kwamba wazee hawa wataweza kulipwa, basi wataweza kujisaidia katika maisha yao."
}