GET /api/v0.1/hansard/entries/1195427/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1195427,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195427/?format=api",
    "text_counter": 271,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, si wazee wa mtaa peke yao ambao wanastahili kulipwa. Wahudumu wa afya katika jamii pia wanastahili kuangaliwa vizuri. Wao pia wanafanya kazi kwa kujitolea bila malipo. Wao pia wanastahili kusaidika. Katika maeneo Bunge, kuna wazee ambao umri wao ni mkubwa na kuna wengine ambao umri wao ni mdogo. Wote bado wanasimamia vijiji vyetu. Sisi tunawapamba tu kwa kuwapatia majina kama mabalozi na mengineyo, lakini majina hayataweza kusaidia. Pesa mfukoni ndiyo itaweza kuwasaidia wazee hawa wa mitaa ili kuona kwamba wanafanya kazi yao katika njia bora. Mhe. Spika wa muda, nachukua fursa hii kusema kwamba kuna zile pesa za wazee. Umri uliowekwa ili wazee waweze kuhitimu kupata pesa hizo ni mukubwa sana. Kwa hivyo, ni vizuri pia Bunge hili lizingatie suala hili. Badala ya kuweka umri wa miaka 65 ama 70 ndiyo waweze kufaidiaka na pesa za wazee, ninapendekeza miaka hii ipunguzwe. Siku hizi shida zimekuwa nyingi. Kufikisha umri wa miaka 60 au 70 ni bahati kubwa sana kutoka wakati wa Yesu. Shida zilizoko siku hizi ni nyingi, na wazee wanakufa wakiwa na umri wa miaka 55 ama 60."
}