GET /api/v0.1/hansard/entries/1195428/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1195428,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195428/?format=api",
"text_counter": 272,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, ninaomba umri wa kupokea pesa za wazee upunguzwe mpaka miaka 50. Pesa hizi zinafaa zije nyanjani, kwenye constituencies, ambako sisi ndiyo tunaweza kuona ni wazee wapi ambao wako katika sehemu zetu ili tuweze kuwatambua na kuona kuwa wanapata pesa zao. Mhe. Spika wa Muda, ninachukua fursa hii, kwanza, kuwashukuru sana wazee wa mitaa katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni ya Jomvu kwa sababu waliniunga mkono na kunirudisha Bungeni kwa mara ya tatu. Mambo niliyowambia nilipokuwa nikifanya kampeni ni haya haya ambayo nayazungumzia hapa Bungeni leo hii – kwamba, ni haki pia wao walipwe. Tukiweza kuyapitisha mambo haya, tutamsihi Mhe. Rais William Samoei Ruto kutia sahihi sheria itakayoundwa kufuatia kupitishwa kwa Hoja, na pesa ambazo zitaenda mashinani kwa malipo yao ziwekwe kwenye Budget haraka iwezekanavyo ili wazee hawa waweze kupata matumaini katika maisha yao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}