GET /api/v0.1/hansard/entries/1195429/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1195429,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195429/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Ninachukua fursa hii kuwaarifu wazee wa mitaa katika wadi za Miritini, Mikindani na Jomvu Kuu kwamba, Bunge hili linazingatia maslahi yao kwa sababu limetambua kwamba wazee hao wanafanya kazi hizi muhimu. Tukiweza kupata pesa za malipo yao wataweza kunufaika. Mhe. Spika wa Muda, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Wacha nisichukue muda mwingi ili niweze kuwapa wenzangu nafasi ya kuweza kuchangia Hoja hii. Vilivile, nampongeza Mbunge aliyeileta Hoja hii ya maana sana. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}