GET /api/v0.1/hansard/entries/1195434/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1195434,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195434/?format=api",
"text_counter": 278,
"type": "speech",
"speaker_name": "North Imenti, Independent",
"speaker_title": "Hon. Rahim Dawood",
"speaker": null,
"content": " Thank you, Hon. Temporary Speaker. Ninaunga mkono Hoja hii ya wazee wa mtaani ama wa vijiji. Pia tunao vijana na wamama wa umri tofatuti tofauti. Wengine wako na umri mdogo ilhali wengine ni wazee. Cha muhimu ni utendakazi na ushauri wao. Hao ndio huwashika wale wauzaji chang’aa ama walio na mambo mengine kama uhusiano wa uhalifu vijijini. Miaka kumi au kumi na tano iliyopita, nilitaka kuwashoneshea mavazi ndio waweze kujulikana kama wazee wa vijiji lakini niliambiwa haingewezekana maana hayo mavazi ni lazima yawe na virauni vya Serikali. La maana ni wao wanafanya kazi zaidi ya machifu na wasaidizi wa makamishna wa kaunti. Mambo yanapoharibika pale vijijini, wao ndio hufanya kazi kuliko manaibu wa chifu, machifu na wasaidizi wa makamishna wa kaunti. Pia, wanapotembea vijijini, wanatumia pesa zao hata usiku ili wafikishe wahalifu kwenye vituo vya polisi waaandikishe statement na mambo mengine mengi. Hii Hoja ambayo imeletwa na Mhe. Mutuse ni nzuri lakini haitatusaidia kwa sababu inapendekezea Serikali iwape pesa na kuwatambua. Sisi kama Wabunge tutengeneze Mswada ambao utawatambua lakini, tusitumie neno “urges” maana haitoshi. Hii ni kana kwamba tayari Serikali haina mpango na haitachukulia maanani hii Hoja. Hii Hoja ikishamalizika, Mhe. Mutuse aipeleke kwa Karani Mkuu ndio tuibadilishe iwe sheria ndio hao wazee wasaidike. Mhe. Spika wa Muda, nimebakisha dakika mingi na ningependa kumpa Mhe. Wa Emgwen, Hon. Lelmengit, hiyo nafasi. Ninaunga mkono. Asante na Mungu awabariki."
}