GET /api/v0.1/hansard/entries/1195473/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1195473,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195473/?format=api",
"text_counter": 317,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ahsante Mhe. wa Kibwezi Magharibi, kwa kunipa nafasi katika muda wako wa kujibu Hoja hii. Hoja hii imekuja wakati unaofaa. Sio mara ya kwanza tunazungumzia Hoja hii. Tulipitisha Hoja hii katika Bunge la Tisa na pia katika Bunge la Kumi na Moja. Ni maombi yangu kuwa katika kipindi hiki, Hoja hii itiliwe maanani na Serikali yetu mpya. Natumai kwamba ikiwa itawezekana, pia wazee wa mitaa wafikiriwe katika ule mfuko wa wachochole ama hustlers na kupewa sehemu ya mfuko huo, ili waweze kupata hata pikipiki za kuwawezesha kufanya kazi yao vizuri. Tukizingatia wale senior village elders, kule kwangu kuna Mzee Magogo ambaye anafanya kazi nzuri sana katika sehemu ya Magarini. Wengi wao wanafanya kazi nzuri. Ikifika wakati wa kugawa chakula, wao ndio huwa kipaumbele kutujuza ni wapi kunahitajika msaada. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}