GET /api/v0.1/hansard/entries/1195694/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1195694,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195694/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika. Ningependa kuweka msisitizo. Msisitizo huu siyo kwa Mwenyekiti wa Tume hii amejilimbikizia faida hizi zote na pesa bila kuangalia sekta nyingine ama watu wengine ambao pia wanapitia changamoto labda hata zaidi yake, bali kwa mtu yeyote ambaye ataweza kuhudumu katika ofisi ya Serikali. Kwanza ajue majukumu na yale mamlaka aliyopewa, si kujipatia yeye mwenyewe binafsi, bali ni kuwafanyia kazi wananchi wa Kenya. Nalaani vikali yeye kuondoa zile fedha ambazo wametengewa Wabunge wa Mabunge ya Kaunti. Sisi tuko huku Nairobi, lakini zile simu na jumbe katika WhatsApp"
}