GET /api/v0.1/hansard/entries/1195707/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1195707,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195707/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Naibu Spika. Jambo la kwanza ni kwamba naonelea hili Bunge la Seneti liweze kujiweka kama Kamati ya Seneti Nzima ili huyu mama wa Tume ya Mishahara na Marupurupu aje hapa ili aweze kujibu maswali kutoka kwa kila Seneta ambaye anahusika. Isiwe Kamati ya Delegated Legislation peke yake. Wachanganyike na Seneti Nzima ili sisi tupate nafasi ya kumuuliza maswali. Jambo la pili ni kuhimiza zaidi ya kwamba askari walio mashinani ni Wabunge wa Mabunge ya Kaunti. Ikiwa benefits na allowances zao zote zimepigwa marufuku ama akazisimamisha na ameziondoa kabisa, watahudumi wananchi kivipi. Mfano ni Sen. (Dr.) Khalwale kule nyumbani Kakamega County, ambaye ako na wengi zaidi. Wabunge hao wote wa Bunge la Kaunti wamepoteza mapato yao yote kwa sababu ya huyu mama, lihali walikuwa wakipata kutoka zamani. Sheria za utendakazi zinasema ya kwamba mshahara ama mapato hayawezi kupunguzwa. Ikiwa huwezi kuongeza, unawacha pale ilipo. Ni jambo la kusikitisha tukiona huyu mama anakigeuza hiyo sheria na akapunguza mishahara na marupurupu mengine."
}