GET /api/v0.1/hansard/entries/1195714/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1195714,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195714/?format=api",
    "text_counter": 217,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipatia mwongozo. Jamba lingine ambalo Bi. Mengich alikosea, hakuongea na mtu yeyote hapa Bungeni kabla ya kutoa uamuzi huu. Lazima kuwe na mashauriano kati ya wale wanaotoa uamuzi fulani na wenye kuathiriwa na uamuzi huo. Sisi tuko hapa. Angetuita kwa public participation tumweleze yetu na yeye atueleze yake, ndio achukue hatua. Sasa amechukua hatua baada ya kujadiliana na nani? Amekiuka Katiba kwa kutojadiliana hili jambo na wahusika. Bw. Naibu Wa Spika, jambo la mwisho ni kwamba hata Wabunge wameathirika sana na huo uamuzi wa Bi. Mengich. Wabunge husafiri katika mataifa mbalimbali. Sasa hivi ukienda Marekani au Afrika Kusini, pesa unazopewa za kugharamia pahali pa kuishi na chakula, zitafanya hata usiende huko. Ni kana kwamba amevunja safari zote ili Wabunge wote waketi tu hapa wala wasiende popote na wasifanye chochote. Kazi yao iwe tu kuja hapa kupokea na kwenda zao mashinani. Hilo siyo jambo nzuri. Maoni yangu ni kwamba, Bi. Sarah Serem aliongoza Jopo la SRC vizuri."
}