GET /api/v0.1/hansard/entries/1195941/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1195941,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195941/?format=api",
"text_counter": 444,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Taratibu za Bunge ni kwamba ikiwa alikuwa anataka kumueleza Sen. M. Kajwang’ kuhusiana na taarifa fulani, alifaa kukuambia kuwa siyo hoja ya nidhamu. Angesema anataka kumfahamisha ili aseme kama amekubali lakini hakumuuliza Sen. M. Kajwang' kama angependa kufahamishwa. Kwa hivyo, yeye ndiye amepotoka. Pili, Sen. M. Kajwang’ amesema jambo muhimu sana. Alisema kuwa Sen. Tabitha Keroche asisahau. Wakati tuko kwenye likizo fupi, ni muhimu kusisitiza kwamba Serikali inafaa kuwajibika kwa sababu serikali za kaunti zinahitaji pesa hizo. Tuko hapa kama Maseneta kwa sababu ya serikali za kaunti. Tunafaa kuwapelekea pesa ili watengeneze serikali zao. Hawawezi kupata pesa tusipoweka taratibu. Kwa hivyo, yeye hakukosea. Alikuwa anawakumbusha walio ndani ya Serikali wafahamishwe kupitia kwa Kiongozi wa Wengi katika Seneti."
}