GET /api/v0.1/hansard/entries/1195959/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1195959,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1195959/?format=api",
    "text_counter": 462,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Naunga mkono na pia ninaeleza ni kwa sababu gani tunahitaji kufunzwa tukienda likizo. Hii ni kwa sababu kuna taratibu ambazo tunafaa kufundishwa kulingana na yale ambayo yamefanywa hapa na maseneta. Najua ya kwamba ndugu yangu, Sen. (Dr.) Khalwale, atakubaliana na mimi. Yeye mwenyewe amesimama hapa akisema tabia kama hio sio nzuri. Seneta anafaa aenda pale, ainame, asimame, alafu aende upande ule anaotaka ama aingie ndani wakati Spika yuko kwenye kiti. Bw. Spika wa Muda, sio hiyo taratibu peke yake ambayo tunafaa kufundishwa. Kuna taratibu nyingi. Ni muhimu hawa ndugu zetu waweze kujua kile ambacho wanafaa kufanya wanapotaka kuongea wakati umeketi hapo. Sisi tumepitia hayo mafunzo kuanzia mwaka wa 2013. Mtaalamu wa taratibu ama Standing Orders zetu za Bunge ni Sen. (Dr.) Khalwale na hakuna mtu anayeweza kumshinda. Yeye ni mtaalamu na mkongwe. Najua ya kwamba tutajifundisha mengi kabla turudi. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hili. Ni jambo nzuri tukienda likizo kwa hizo siku nne ama tano ili tuweze kufundishwa mambo ya taratibu za hapa Bunge. Tukirudi, tutakuwa tumenoa kabisa msumeno ya kufanya kazi ndani ya Bunge la Seneti. Asante sana. Naunga mkono."
}