GET /api/v0.1/hansard/entries/1196084/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1196084,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196084/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Nampongeza ndugu yangu na kipenzi, Mhe. Duale. Pongezi sana, maanake likija kwetu lazima tutaskia raha. Nina imani kuwa mipaka yetu itakuwa salama katika mikono yako. Nina imani kuwa wanajeshi wataskia raha katika mikono yako. Nina imani kuwa ulinzi katika taifa hili utaimarika. Kwa dada yangu kipenzi, Mhe. Alice Wahome, maji ni donda sugu katika taifa hili. Tumeona ndugu zetu wa North Eastern wakilia. Nina imani, kama mama, kuwa utaweka vizingiti na maji yaenee sehemu zile watu na wanyama wanakufa kwa ajili ya njaa. Hii ni ili Kenya iwe kijani kibichi sehemu zote za Kenya ambazo ni kavu. Nawashukuru sana na nawaombea dua. Ndugu yangu Duale, shika kazi, shika kasi. Nitaubisha mlango wako hivi karibuni. Asante sana, Mhe. Spika. Kwa niaba ya Mombasa, nawaambia nyote kongole."
}