GET /api/v0.1/hansard/entries/1196132/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1196132,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196132/?format=api",
    "text_counter": 134,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Naibu Spika wa Muda. Kwa majina natambulika kama Amina Laura Mnyazi, Mbunge wa Eneo Bunge la Malindi. Jambo la kwanza ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha hapa. Vile vile, nashukuru watu wa Malindi kwa kuwa na imani nami kwa kuniteua kama Mbunge wao. Najua hili jukumu ambalo liko mbele yangu ni jukumu kubwa. Namuomba Mwenyezi Mungu aweze kunisimamia ili niweze kutekeleza yale yaliyoko mbele yangu. Ningependa kuwapongeza Mawaziri wote waliopitishwa leo. Pongezi sana. Jukumu kubwa liko mbele yenu. Pongezi zangu haswa zimfikie dada yangu, Mheshimiwa Aisha Jumwa, ambaye nimekalia kiti chake kwa sasa. Kumekuwa na mambo mengi, lakini namuunga mkono. Anatoka Eneo Bunge langu, na namuombea kila la kheri ili aweze kuzidi kufungulia milango wanawake wote wa Kaunti za Malindi na Kilifi. Mhe. Spika wa Muda, lingine ni kuhusu yale matatizo ambayo yanakumba Eneo Bunge la Malindi kama baa la njaa. Kama munavyoona, matatizo ya chakula na baa la njaa yamefika kila mahali katika Kenya hii. Sisi pale Malindi, kuna Mswada tulipendekeza ambao unafahamika kama Kavunyalalo Irrigation Scheme. Mpaka kwa dakika hii, hatujaelewa ni kwa nini pesa zile hazijafika mashinani ili watu waweze kujisaidia. Nataka nieleze wazi hapa ya kwamba tunahitaji mradi kama huu ndani ya Eneo Bunge la Malindi ili tuweze kujiendeleza kupata pato la chakula na kuondoa baa la njaa."
}