GET /api/v0.1/hansard/entries/1196133/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1196133,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196133/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Malindi, ODM",
"speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
"speaker": null,
"content": "La pili ni masuala ya utalii. Leo niko na raha kwa sababu tunaona dada yetu, msomi, ambaye amefanya kazi katika sekta tofauti. Jina lake limepitishwa kama Waziri wa Utalii. Ninataka nimpongeze dada yangu huyu na nimwambie awe macho na makini. Zile sheria ambazo zinapitishwa hapa Nakuru ama Nairobi, haziwezi kuwa sawasawa zipitishwe pia kule Malindi. Huu ni mji ambao tumetegemea utalii kwa muda mrefu. Tunataka tufanye kazi na kupitisha miswada ambayo itapendekeza na itapendelea ile hali ya watu wa Malindi wanapofanya kazi pale."
}