GET /api/v0.1/hansard/entries/1196137/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1196137,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196137/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": "Donda sugu ambalo limeathiri Eneo Bunge la Malindi mpaka kwa sasa ni masuala ya ardhi. Hivi ninavyozungumza, uskwota umekithiri ndani ya Malindi. Ndio maana nataka nifanye kazi na wenzangu kuhakikisha kwamba watu wameweza kupata hati miliki zao. Wiki mbili zilizopita, kuna watu wangu zaidi ya 200 ambao nyumba zao zilivunjwa sehemu ambayo inaitwa Pendukiani ndani ya wodi ya Ganda. Jambo kama hilo hatupaswi kuwa nalo katika karne hii na muda huu wa sasa. Hayo ni mambo ambao tunataka tuyaweke sawasawa, ili kuhakikisha tumeweka vitu vyetu sawa na watu wa Malindi wameweza kupata huduma."
}