GET /api/v0.1/hansard/entries/1196138/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1196138,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196138/?format=api",
"text_counter": 140,
"type": "speech",
"speaker_name": "Malindi, ODM",
"speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
"speaker": null,
"content": "Kuna wale ambao wamezungumza kuhusu Hoja ya walimu ambao wanahamishwa na kupelekwa kaunti zingine. Naunga mkono Hoja hiyo. Walimu wa Malindi wamezungumza kwa sauti moja na kusema niunge mkono Hoja hiyo. Delocalisation imeleta more harm thangood to the teachers. Walimu wamewacha na kuvunja familia zao. Kuna athari nyingi ambazo zinakuja juu ya haya matatizo. Sisi tunataka tupitishe Miswada ambayo itawezesha Teachers Service Commission (TSC) kufanya kazi na Kenya National Union of Teachers (KNUT), Kenya Union of Post-Primary Education Teachers (KUPPET) na wadau katika sekta ya elimu, ili kuhakikisha walimu wanahamishwa na mpangilio barabara ambao unafuatiliwa, ili watu wasisumbuke katika mahitaji yao ya hapa na pale."
}