GET /api/v0.1/hansard/entries/1196199/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1196199,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196199/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuiunga mkono Hoja hii na kusema kuwa mikakati maalumu inapaswa iwekwe katika tume hii ya TSC kulingana na vilio vya walimu wengi kote nchini. Kwanza, nitazungumzia Eneo Bunge langu la Nyali. Sisi Wabunge wa Taifa tuna majukumu makubwa sana ya kuwekeza katika elimu. Kadri tunavyozidi kusonga mbele na kujenga shule hapa na pale katika wadi mbalimbali, tumekuwa na changamoto sana ya uhaba wa walimu. Vile vile, wakati walimu wanaandikwa kazi, hawaandikwi kutoka maeneo yetu. Ni kana kwamba njia ambayo TSC inatumia inafaa kupigwa msasa na kuhakikisha kwamba maswala yote yanayohusu walimu wa Jamhuri ya Kenya yanaangaliwa kwa undani na umakini kabisa. Tukizungumzia kazi zao, watu kuondolewa katika maeneo yao na kupelekwa katika maeneo mengine bila sababu… Wakati wa kuajiri, unashtukia kuwa ni watu kutoka sehemu zingine wanaoletwa katika sehemu zile na kuwacha walimu ambao wako pale. Jambo hilo linafanya shule ambazo sisi tumejenga kama Wabunge kuwa na uhaba wa walimu na kutegemea wale wa Board of Management (BOM). Vile vile, ningependa kuzungumzia TSC yenyewe. Kama Mbunge katika Bunge la 12 lililopita, nilikuwa na wakati mgumu sana, hususan nikienda katika afisi zao kutafuta usaidizi, sanasana tunapojenga shule na kuhakikisha kwamba tunataka walimu wa kutosha. Ukienda katika majengo yao, Tume hiyo inaendeshwa kama gari la wizi. Ni Tume ambayo haitaki kusikiliza. Haiwaheshimu Wabunge, na haitaki kusikia vilio vya watoto wa maeneo bunge kwa sababu vilio vyao ni vya uhaba wa walimu. Ni vilio vya walimu kulipwa mishahara duni. Ni vilio vya walimu ambao hawana hata bima ya afya inayoweza kuwasaidia vizuri. Ni vilio vinavyosababisha watoto kupata alama za chini katika maeneo bunge ama kaunti mbalimbali humu nchini. Uhaba wa walimu unasababisha alama mbaya. Kutumia walimu wa BOM na kukataa kuajiri walimu bado inazidi kuleta mzigo. Walimu wakubaliwe kuchukuliwa katika sehemu zao. Wao pia ni binadamu. Najua kuna ule mpangilio wa asasi za Serikali ya kwamba mtu akifanya kazi katika kipindi fulani katika kituo fulani, kwa muda fulani, ni sharti aondolewe apelekwe sehemu nyingine. Lakini utapata katika hii TSC, sio hivyo. Wao wataendesha vile wanavyotaka. Sisi kama Wabunge tuna majukumu makubwa sana. Kwa mfano, katika kipindi cha miaka mitano cha Bunge la 12 lililopita, niliweza kujenga shule takribani saba kule Nyali. Mpaka wa leo katika Bunge la 13, hizi shule saba zinaendeshwa na walimu watatu wa BOM."
}