GET /api/v0.1/hansard/entries/1196208/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1196208,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196208/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon Zamzam Mohammed (",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mombasa CWR, ODM): Asante sana Bwana Spika wa Muda. Nashukuru sana kwa Hoja ambayo imeletwa na ndugu yangu Mhe. Khamala kuhusu kuhamishwa kwa walimu kiholelaholela. Ni dhairi kwamba walimu wamepitia mitihani mikubwa. Wengine wameshikwa na msongo wa mawazo kwa sababu kila wakihamishwa na kupelekwa sehemu za mbali wakati wamejidhibiti katika sehemu moja, inakuwa matatizo kwao kwa sababu hata mapeni pia wakati wanapata dharura nyumbani inakuwa ni mtihani kusafiri. Kwa hivyo, ningependa kumuunga mkono ndugu yangu Mhe. Khamala kwa Hoja hii na kusema walimu wana haki na TSC isiwafanye kama mpira wa kona kuchengwa huku na huku na kuwasumbulia maisha yao. Kwa hivyo naunga Hoja hii kuwa walimu waweze kupewa nafasi ya kufanya kazi popote wanapotaka wao wenyewe. Asante sana."
}