GET /api/v0.1/hansard/entries/1196290/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1196290,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196290/?format=api",
"text_counter": 292,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii kwanza, kuwashukuru ndugu zangu wa Mombasa kwa fursa ambayo wamenipa kuwawakilisha katika Bunge hili. Nawahakikishia kuwa nitafanya kazi kwa uadilifu. Kuna tashwishi sana kule mashinani kuwa hatujafikisha pesa za National Government Affirmative Action Fund (NGAAF). Nawaambia kuwa bado NGAAF haijapitishwa kama vile National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF) ilivyopitishwa. Kwa hivyo, mkiona Wabunge wenu, vumilieni. Msiwapige mawe Wabunge, kwa sababu bado hawajapata pesa. Natumai pia Wabunge walio hapa wana shida kama hizi. Ningependa kuunga mkono Hoja hii ya wazee wa mitaa. Wazee wa mitaa wamejitolea sana katika maisha yao na wamepata changamoto sana. Ukiangalia kesi za watu wanaopigana kama mama na baba, ni wao huitwa. Ukiangalia kesi za watoto kupotea, ni wazee wa mitaa wanaozishughulikia. Ukiangalia kesi za wahalifu na majambazi, ni wazee wa mitaa ndio wanaweza kuwatambua. Wanafanya kazi hata zaidi ya polisi. Ningependa kueleza Serikali kuwa ni makosa kuwatumia hawa wazee kufanya kazi kule mitaani. Wao wanalipa ushuru na wananunua kila kitu, huku hawapati mishahara. Ningependa kuomba Serikali ichukue kilio cha wazee wa mitaa na kuweza kuwalipa kama machifu na mapolisi ili hao pia waweze kunufaika pamoja na familia zao. Tunawahitaji sana wazee wa mitaa kwa habari tendeti, kusuluhisha matatizo mengi kule mitaani na mashinani. Najua mpaka sasa wao hawana malipo yoyote na wengi utapata hata hali zao za kiafya ziko pabaya. Maanake, mzee wa mtaa licha ya kuwa anafanyia Serikali kazi anashindwa hata kulipa pesa ya National Health Insurance Fund (NHIF) kuweza kujisaidia. Ni hatia na mimi naona ni aibu sana kwa Serikali kutumia wazee kama wale kupeana huduma kule mitaani ilhali wanaachwa bure. Wakati mwafaka umefika ili wazee wa mitaa wawekwe akilini na wapewe hata kama ni mshahara japo mdogo. Sharti mara hii wakumbukwe na Serikali. Sina mengi ya kusema kwa sababu muda haunasi. Nasapoti Hoja hii. Naiunga mkono. Kutoka Mombasa Kaunti ni mama Zamzam Chimba Mohammed. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii."
}