GET /api/v0.1/hansard/entries/1196381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1196381,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196381/?format=api",
    "text_counter": 81,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia North, JP",
    "speaker_title": "Hon. Sarah Korere",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "kupigwa msasa na darubini waliopitia kwa wananchi haikuwa kazi rahisi. Kazi ya Bunge hili ni kuwapiga msasa wale waliopendekezwa na Rais kuwa mawaziri kwa sababu ya ustawi na maendeleo ya jamii ya Kenya. Mheshimiwa Spika wa Muda, kazi inayomsubiri Rais wetu mpendwa wa nchi hii ni kubwa inayohitaji uadilifu na uaminifu, na bila shaka haiwezi kufanywa na watu ambao maadili yao yana tashwishi. Kutoka kwa jamii ya wafugaji, ningependa kumpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa maana ninapotazama watatu ambao wameteuliwa katika jamii ya wafugaji, akiwepo aliyekuwa Kinara wa walio wengi Bungeni, Mheshimiwa Aden Bare Duale, bila shaka maadili yao sio ya kutiliwa shaka ama tashwishi yeyote. Na zaidi ya hayo, ni watu ambao wako na utu na ubinadamu. Kwa mfano, ukimtaja Mheshimiwa Soipan Tuya, tangu Mungu alipoumba dunia haijatokea mwanamke wa jamii ya kimasaai kuwa waziri katika nchi ya Kenya. Uteuzi wa Mheshimiwa Soipan Tuya sio bora mama, bali ni mama bora. Hata kama tunataka akina mama wawe mawaziri na viongozi, hatuwezi kusema bora mama tu, bali ni mama bora. Mheshimiwa Spika wa Muda, ukiangalia huyo msichana wa kimasaai, ni mwanasheria, amekuwa Mbunge katika Bunge hili, na ameweza kuendeleza maendeleo mengi katika Kaunti ya Narok. Ningependa kusema hivi: Ili Rais wetu aweze kushukisha bei ya unga na mafuta, ni sharti tupambane na ufisadi katika nchi hii. Na haitakuwa jambo bora kupitisha tu na kufanya Bunge hili kuwa mahali pa kupiga muhuri kila kitu. Wakenya wanatutazama, na wameweka matumaini yao kwetu. Sasa hivi, hali sio hali tena; wananchi wengi kule Kaskazini mwa nchi wanalala bila chakula, na watu wanakufa njaa. Ukiangalia hali ya usalama, imekuwa si hali tena kwa sababu ya wizi wa mifugo na mauwaji ya kiholela. Kwa hivyo, wanaochukua nyadhifa hizi ni lazima wapigwe darubini sawasawa, na wawe watu ambao watakaohakikisha kwamba Wakenya watapata haki zao."
}