GET /api/v0.1/hansard/entries/1196382/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1196382,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196382/?format=api",
"text_counter": 82,
"type": "speech",
"speaker_name": "Laikipia North, JP",
"speaker_title": "Hon. Sarah Korere",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "Mheshimiwa Spika wa Muda, nilikuwa natazama Katiba ya Kenya asubuhi hii, na Sura ya Nne inazungumzia haki ya Mkenya. Baadhi ya haki iliyozungumziwa ni haki ya Mkenya na mali yake kuwa salama. Lakini sasa hivi, wananchi wa Kitui wanahangaishwa na Wakenya wenzao. Ukitazama Laikipia Kaskazini, tunahangaishwa na majambazi wanaotoka kaunti jirani. Wengi wetu tumepokonywa haki yetu tuliyopewa na Katiba ya Kenya; haki ya mali na nafasi yetu kulindwa. Haki nyingine ambayo Wakenya wengi wamepokonywa ni elimu ya msingi, ambayo ni haki ya kila mtoto Mkenya. Mheshimiwa Spika wa Muda, leo hii ukitembea Kaunti ya Baringo, haswa eneo Bunge la Tiaty, ambao ni majirani wangu, utapata kwamba miongoni mwa wale watu, zaidi ya asilimia sabini hawawezi kusoma wala kuandika. Lawama sio kwao, bali kwa Serikali ambayo imepokonya haki yao ya kimsingi ya elimu. Serikali inapowanyima wananchi wa Kenya haki zao za kisheria, inastahili wananchi hawa waishtaki Serikali yao. Naomba Mwenyezi Mungu kuwa wale watakaokuwa mawaziri, haswa wa Elimu na Usalama, watahakikisha kwamba tunarejeshewa haki zetu tulizonyimwa kwa miaka na mikaka. Sura ya Sita ya Katiba ya Kenya inazungumzia maadili yanayoambatana na utumishi wa umma na watumishi wa umma. Mimi naomba Mungu kuwa hivi karibuni, tutaona Wakenya wenyewe wakikataa kuteuliwa iwapo wanajua wana madoadoa. Kuna baadhi yao ambao wana doa kulingana na maadili yao. Mimi kama mama sijui vile nitaingia kwa ofisi ya mtu aliye na shutuma ya ubakaji; nitakuwa na hofu sana. Ingekuwa jambo la busara iwapo ndugu zetu katika Kenya Kwanza wamekosa watu wenye maadili mazuri, wangetuomba upande huu, kwa kuwa tuna watu wengi. Nasema hivi kwa sababu singetaka kusikia eti mwanamke ameenda kutafuta kazi ama kutumikiwa katika ofisi ya umma kisha akabakwa. Mimi nina hofu na baadhi ya wengine wao. Ijapokuwa sitawataja, lakini wapo. Iwapo mtu amekiri kuwa ana kesi 35, hata akitunukiwa ile nafasi, akili yake haitatulia. Hataweza kututumikia akiwa na akili tulivu. Ijapokuwa ako na kesi haimaanishi kuwa ametenda yale makossa. Sasa hivi, anastahili apewe The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}