GET /api/v0.1/hansard/entries/1196383/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1196383,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196383/?format=api",
"text_counter": 83,
"type": "speech",
"speaker_name": "Laikipia North, JP",
"speaker_title": "Hon. Sarah Korere",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "nafasi ili azishughulikie kesi zake 35 halafu nafasi hii ipatiwe Wakenya wengine wasio na doa, kasoro wala tashwishi ili waweze kuwatumikia Wakenya . Nikirejelea swala la Bi. Peninah Malonza, huyu mwanamke maskini analaumiwa kuwa hakuweza kuzungumza. Sio mara ya kwanza kwa wanawake kulaumiwa. Katika shamba la Edeni, Adamu ambaye alitangulia kula tunda walilokuwa wamekatazwa kula katika hilo shamba, alimlaumu Hawa kwa kosa lake, ilhali yeye ndiye aliyetangulia pale. Ni yeye angekataza lile tunda kuliwa. Wanataka kumfanya binti Malonza kama kafara bure. Iwapo ni kupita, basi sharti huyu binti pia apitishwe. Shukrani, Mheshimiwa Spika."
}