GET /api/v0.1/hansard/entries/1196770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1196770,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196770/?format=api",
    "text_counter": 146,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kumpa mkono wa buriani, Sen. Murkomen, ambaye amekuwa na sisi hapa kwa muda wa miaka kumi. Nilipoingia Bunge hili la Seneti mwaka wa 2017, Sen. Murkomen alikuwa ni Kiongozi wa walio Wengi katika Bunge hili. Kwa hakika, aliwahudumia Maseneta wote kwa njia ya usawa. Na kwamba hakuwa na ubaguzi wa aina yoyote. Natumai, Sen. Cheruiyot, pia ataweza kusoma somo hili na aweze kuendeleza mkondo huu ambao ulikuwa unawasaidia Maseneta wote. Vilevile, katika Bunge, tumecheza mechi nyingi sana na Sen. Murkomen. Hususan, mechi ya kwanza kabisa tulicheza kule Machakos ambako alifunga bao la kichwa kutokana na pasi ambayo mimi nilimpatia. Na hiyo ikamfanya kuwa mchezaji mkubwa sana kule Elgeyo-Marakwet mpaka kila mtu akamtaka awekwe katika Timu ya"
}