GET /api/v0.1/hansard/entries/1196824/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1196824,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196824/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa ili nimpe mkono kakangu, Sen. Murkomen, na kumtakia kila la heri katika nafasi yake ya Waziri wa Barabara, Usafiri na Ujenzi. Ndugu yangu, Mhe. Murkomen, kuna kitu ambacho ningependa uzingatie sana. Huwezi kutoka Kaunti ya Mombasa hadi ya Kwale, bila kupitia Mombasa. Kivuko pekee ni pale Feri na hapo pana shida kubwa sana. Mwaka juzi kulitokea ajali mbaya sana ambapo gari lilitumbukia baharini. Ni kwa sababu hakuna watu wa kuangalia usalama katika Feri. Mimi ninaomba Mungu akujalie uapishwe, kisha ninakuomba uandamane na viongozi wa Pwani, uje Kenya Ferry uone vile watu wanavyohatarisha maisha yao katika hicho kivuko. Kila siku nikivuka, huwa ninaomba Mwenyezi Mungu tuvuke salama. Wananchi hawana usalama ndani ya Feri wanapovuka. Unakuta watu wanaingia katikati ya magari, Feri zinaondoka na ni mbovu na foleni ni ndefu hadi karibu barabara ya Kizingo. Ninamsihi Sen. Murkomen aangalie hili jambo la Kenya Ferry. Pia kuna mambo ya Bandari ya Mombasa. Hii Bandari iko na shida sana kwa sababu ufisadi umezidi. Tunataka usafishe huo ufisadi. Katika Kaunti ya Kwale, kuna Bandari ya Shimoni ambayo tunataka kujengewa. Kakangu, Mhe. Murkomen, tutabisha milango kila mara kukuambia kwamba hii Bandari isimamishwe sawasawa. Ninamtakia kila la heri na tutakua tukibisha milango kila mara kumkumbusha habari ya Kenya Ferry na Bandari ya Shimoni. Mungu akubariki."
}