GET /api/v0.1/hansard/entries/1196850/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1196850,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196850/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa nafasi hii kumpongeza Waziri Murkomen. Waziri Murkomen amethibitisha kwamba ukifanya kazi yako vizuri kikamilifu katika Seneti, unaweza kufika kiwango tofauti. Kwa hivyo, huo ni mfano mwema kwa viongozi wengine. Wameweza kuona ya kwamba mtu anaweza kutoka pale alipo na akasonga mbele. Sen. Murkomen amethibitisha hivyo. Mhe. Waziri, najua umepewa maombi mengi tofauti na watu. Nikiongezea sauti yangu, sisi watu wa Lamu hatujawahi kupata lami. Labda, kama LAPSET haingekuwepo, hatungekuwa hata na kilomita moja ya lami. Lami hiyo imewekwa upande wa Lamu Magharibi. Tunakuomba, Sen. Murkomen, uweze kutuwekea lami upande wa Lamu Mashariki; kutoka LAPSET hadi Kiunga, kwa sababu hiyo ndiyo barabara ambayo magaidi hutumia wakija kufanya uhalifu katika Kauti ya Lamu. Mhe. Murkomen, ukitengeneza hiyo barabara itokayo Hindi hadi Kiunga mpaka Mkokoni, utakuwa umetupunguzia mzigo mkubwa sana wa magaidi na tutakuwa tunapita barabara hiyo bila shida yoyote. Bw. Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii. Nampongeza sana Sen. Murkomen. Sina shaka atawacha urithi wa kuthibitisha kwamba ameweza kufanya kazi katika hiyo Wizara kwa kufanya kazi nzuri."
}