GET /api/v0.1/hansard/entries/1196852/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1196852,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196852/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika, asante kwa kunipa nafasi hii. Jambo la kwanza, nampa kongole ndugu yangu Sen. Murkomen, kwa kuteuliwa kama Waziri. Hatimaye, Bunge la Kitaifa limepitisha kwamba anafaa na anastahili kuwa Waziri wa Barabara, Uchukuzi na Ujenzi. Nampa mkono wa buriani ndugu yangu Sen. Murkomen. Bw. Naibu Spika, kama ndugu yake mkubwa kwa umri, ningependa kumwambia kwamba wadhifa aliopewa ni mkubwa sana. Macho yote yatamwangalia. Watu hawataangalia umri bali wataangalia matendo ambayo atatenda ofisini. Namuomba ashike vizuri sana wasia ninayo mpa na ayafunge katika vidole vyake. Wasia wenyewe ni atumikie Wakenya wote kwa roho mmoja. Ninayo imani kwamba atawatumikia kwa uwezo na maarifa, kadri ya mwenyezi Mungu alivyompea. Jambo la muhimu ambalo linakumbukwa na Wakenya wengi waliweza kuliona, ni tendo lake wakati wa ugavi wa pesa. Mimi nilikuwa shahidi. Seneta wa Nandi alitutoroka na alikimbia mbio sana. Wakati huo, sisi watu wa Kilifi tulikuwa tunapoteza pesa, Tana River, na Kaunti zingine pia zilikuwa zinapoteza pesa. Lakini, Sen. Murkomen na Sen. Cheruiyot---"
}