GET /api/v0.1/hansard/entries/1196867/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1196867,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1196867/?format=api",
"text_counter": 243,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Ni vyema Sen. Murkomen ajue ya kwamba, wakati atapoketi katika Wizara akiendeleza utendakazi wake, watu wa pwani watakuwa wanamuangalia. Tumetazama Serikali zilizopita, kutoka wakati wa Uhuru mpaka hivi sasa, ambapo Serikali inaongozwa na Mhe. Rais Ruto. Wakati watapokuwa wanafikiria kutengeneza barabara za pwani, wasifikirie tu mambo ya utalii. Hilo ndilo lilikuwa lengo la hizo serikali zingine. Tuanze kufikiria kwamba watu wa pwani pia wako na marikiti, masoko makubwa na ni wakulima ambao wanahitaji barabara ili waweze kwenda vitongoji, kule wanapoishi. Hiyo itakapotendeka, hata sisi tutaweza kupata maendeleo kama kaunti zingine za Kenya."
}