GET /api/v0.1/hansard/entries/1197179/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1197179,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1197179/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kamukunji, JP",
"speaker_title": "Hon. Yusuf Hassan",
"speaker": {
"id": 398,
"legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
"slug": "yusuf-hassan-abdi"
},
"content": " Asante, Bw. Spika, kwa kunipatia fursaa hii ili nitoe ilani ya Hoja kuhusu kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kitaifa. Bw. Spika, naomba kutoa ilani ya Hoja ifuatayo: KWAMBA, tukitambua Kifungu cha 7 cha Katiba ya Kenya kinabainisha Kiswahili kuwa lugha pekee ya kitaifa, na pia lugha rasmi pamoja na Kiingereza, na aidha kwamba Serikali ina wajibu wa kulinda, kuendeleza na kukuza matumizi ya lugha za kiasili za watu wa Kenya; KUWA Vifungu vya 119 na 137 vya Mkataba wa Uanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vinawajibisha dola za Afrika Mashariki kustawisha na kuendeleza Kiswahili kama lugha ya mshikamano wa nchi wanachama; KWAMBA Mkutano wa 21 wa Marais wa nchi za Afrika Mashariki uliridhia Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwajibisha Tume ya Kiswahili Afrika Mashariki (East African Kiswahili Commission) kuwezesha kukoleza matumizi ya Kiswahili katika kanda hii; na KWAMBA Kiswahili ni moja ya lugha rasmi za Umoja wa Afrika, na kwamba Umoja wa Mataifa kupitia UNESCO umetenga kila Julai 7 kuwa Siku ya Kiswahili duniani; TUKIFAHAMU nchi ya Tanzania iliunda Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) mwaka wa 1967 na Zanzibar ikaanzisha Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) mwaka wa 2004 kwa madhumuni ya kukuza, kuimarisha na kuendeleza Kiswahili eneo la Tanzania bara pamoja na visiwa vya Zanzibar; IKIFAHAMIKA Kiswahili ni lugha asili kwa jamii za Mkoa wa Pwani nchini Kenya na pia Wakenya wengi ni wazungumzaji wa Kiswahili; TUKIJUA lugha ya Kiingereza ina nguvu sana katika mawasiliano rasmi na hivyo kuchangia kudhoofika kwa lugha yetu ya Kiswahili; TUKITAMBUA uamuzi wa mkutano wa tatu wa Baraza la Mawaziri wa Kenya uliofanyika tarehe 14 Agosti 2018 ulioidhinisha kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya kulingana na Kifungu cha 137 cha Mkataba wa Uanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki haujatekelezwa; BUNGE hili linahimiza Serikali Kuu—kupitia Wizara ya Michezo, Utamaduni na Mirathi, kwa ushirikiano na vyombo vya kitaifa na vya kibinafsi vinavyohusika na uboreshaji wa lugha ya Kiswahili—kuanzisha rasmi Baraza la Kiswahili la Kenya na kuzindua mikakati, mbinu na sera mahususi zinazohitajika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Bw. Spika, kama Mbunge wa eneo la Kamukunji, ninakushukuru kwa kunipa fursa hii ili niwakilishe Hoja hii katika Bunge la Taifa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}