GET /api/v0.1/hansard/entries/1197215/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1197215,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1197215/?format=api",
    "text_counter": 101,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika. Nachukua nafasi hii kumpongeza Mhe. Elsie kwa kuleta Hoja hii. Ni wazi na dhahari kwamba katika shule nyingi, haswa za msingi, watoto wengi hawaendelie na masomo kwa ajili ya janga la njaa. Wakati mwingi utawapata wanahudhuria asubuhi na saa nane hawarudi shuleni kwa sababu hawawezi kumudu hali hii ya njaa. Wale wachache wanaoweza kurudi shuleni pia utawapata wanalala, hawana wakati wa kusikiza kwa makini yale wanayofundishwa. Mhe. Spika, ningeomba mara tu Hoja hii inapopita, Kamati ya Utekelezaji wa Hoja kama hii ichukue hatamu na kuhakikisha kuwa inatekelezwa."
}